Jumatano, 4 Juni 2014

BOKO HARAM YAENDELEA KUFANYA MASHAMBULIZI NIGERIA




20 wameuawa katika mashambulio vijiji vya jimbo la Borno Nigeria

 Nigeria imekuwa na kipindi kigumu cha matukio ya kutishia amani yanayoongozwa na kundi la boko haramu kwa muda mrefu sasa bila ufumbuzi wa aina yoyote kutokana na mazingira ya matukio yenyewe yanavyopangwa na kutokea Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50 zilizopita.


Wakaazi wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu waje katika uwanja wa kanisa.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia  kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.

Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete. nyumba zimechomwa Borno


Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio yaliyochacha.Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.

Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka.Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa.

Jumapili, 30 Machi 2014

MAITI 10 AJALI ILIYOTOKEA HEDARU ZATAMBULIWA




Kamanda Boaz athibitisha  watu 10 kufa papo hapo

Abiria hao walikuwa wanasafiri na gari dogo aina ya Toyota Pick Up namba T 170 AKZ kwenda kuhani msiba uliotokea katika kijiji cha Kongei kilichoko Hedaru mkoani Kilimanjaro.

 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro , Robert Boaz waliofariki ni Stella John (45), Salma Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George, (29), Sophia Mbike (51), Ritta Kallani (55) na Kallan Stephano (55), Kolina Mmasa (55) na Bahati Daudi (25),
Wengine ni Farida Kiondo (24) na Maria John (33) wote wakazi wa Kongei na kwamba miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Same.

Boaz aliwataja majeruhi kuwa ni Zubeda Mrindoko (42),Mipa Chediel (29) na Zubeda Mlita (32) ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.Wengine waliolazwa hospitalini Same ni Joyce Kandogwe (29), Subira Juma (22), Ramadhan Msangi (31) na Adinan Rajab (31).
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:00 usiku katika barabara kuu ya Tanga-Moshi, nje kidogo ya mji wa Hedaru, ikihusisha magari matatu ambayo ni Fuso (T 299 ANM) ikitokea Moshi kwenda Dar es Salaam na Scania (T 737 AKW) pamoja na tela lake namba T 776 CCN ikitokea Dar es Salaam kwenda Moshi, kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi.

Alisema watu hao walikuwa wamepanda gari la Diwani wa Kata ya Hedaru (CCM), Gerald Gwena aliyekuwa amewapakia waombolezaji hao kwenye pick-up yake ambayo iligongwa kwa nyuma na Fuso na baadaye gari hilo kuparamiwa kwa nyuma na Scania na kisha kusababisha vifo na majeruhi.
"Waombolezaji hawa walikuwa wanakwenda na diwani kuifariji familia ya marehemu mzee Mwanga ambaye mtoto wake wa kiume, Dismas Mwanga alifariki baada ya kusombwa na mafuriko”, alisema.

Alisema Dismas mwenye miaka tisa aliyekuwa anachunga kondoo milimani alifariki dunia juzi mchana baada ya kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha mfululizo.
Alisema hata, hivyo mpaka sasa haijafahamika iwapo mvua hizo zimesababisha vifo na hasara nyingine.
Kapufi alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imekutana kwa dharura kujadili ajali hiyo na hatua ambazo wilaya hiyo itachukua.

Kamanda Boaz, alisema chanzo cha ajali hiyo ni kuzimika ghafla kwa  gari hilo mali ya diwani Gwena ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo.
"Ajali hiyo ilitokea baada ya gari hilo kuzimika na Fuso iliyokuwa karibu kuteleza barabarani baada ya kujaribu kusimama ili isigongane na Pick Up iliyokuwa na waombolezaji, lakini lilivutwa na tope lililokuwa limejaa barabarani kisha kugonga kabla ya kupinduka na kuangukia upande wa kulia wa barabara ambako kulikuwa na lori la Scania.

Kamanda alisema watu 10 walikufa papo hapo , wawili walifia hospitalini na saba wamejeruhiwa.
Alisema juhudi za kuwasaka madereva  hao wa Fuso pamoja na diwani huyo zinaendelea.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Jumatatu, 24 Machi 2014

IJUE HISTORIA YA MBUNGE WA SAME MAGHARIBI -DAVID MATAYO DAVID

 

David Matayo alikuwa ni mwanafunzi pekee aliyekuwa na radio yenye double deck, (system) na TV set akiwa SUA morogoro wakati anasoma


Jina Jina la kwanza ni Mathayo David Msuya. Ila baada ya kuingia anga za siasa, aliamua kulibadili jina lake kuwa Mathayo David Mathayo na kuondoa jina la ukoo "Msuya" ambalo ni jina la baba yake halisi David Msuye aliyewahi kuwa waziri mkuu. Masomo
Matayo David Msuya alisoma Tosamaganga Iringa, alifanya CBG (1989-91) aliishi bweni la Mwenge. Uwezo wake wa kimasomo haukuwa mkubwa ila alishangaza wenzanke na waalimu alipopata daraja la kwanza kwa pointi 7. Alipata msaada sana kutoka kwa kaka yake aliyekuwa akifundisha chuo cha ualimu Mkwawa, Iringa.
Matayo ulikwenda JKT itende, Mbeya. Baada ya hapo, alichanguliwa kwenda kusoma Makerere Uganda kwa kupitia mfuko wa mwalimu Nyerere. Mathayo alinufaika kwa fedha hizo ila hakwenda Uganda, akaamua kusoma SUA ya tiba ya mifugo (Bachelor of Veterinary Medicine) mwaka 1993-1997. Huko SUA Matayo alikuwa ni mwanafunzi pekee aliyekuwa na radio yenye double deck, (system) na TV set. Uwezo wa kifedha ulisaidia kumpa Mathayo maisha ya kifahari chuoni SUA ambapo alikuwa na wasichana kadhaa ikiwa ni pamoja na Mugros na Betty Manase

Mwanzo wa siasa
Siasa alizianza rasmi mwaka 1995 alitumia TV yake kwenda kuonyesha vijijini madhara ya vyama vingi, alitumia mapigano ya Rwanda na Burundi kama kutishia wananchi wasikubali upinzani na kipindi kile wananchi walikuwa wepesi kuelewa kumbuka TV hazikuwa nyingi Tanzania kipindi kile. Alijijengea umaarufu sana ndani ya chama mkoani Morogoro na kitaifa. Aligombea ujumbe wa NEC mkoa wa Morogoro kundi la vijana alishinda. Mathayo alimaliza SUA 1997 na kupata kazi ya kufundisha chuo kimoja huko Serowe Botswana. Kwa kuwa mjumbe wa NEC alikuwa karibu na akina Lowasa, JK na vingunge wengine aliweza kuwa anaonana na akina Makamba na akawa ni mwanamtandao. Wakati huo Matayo alikuwa akirudi Tanzania kufanya shughuli zake za kisiasa wakati bado ni mwajiriwa wa serikali ya Botswana. Kwa mfano wakati mmoja alirudi Tanzania na kuwahamasisha wanafunzi wa SUA (kama 200 hivi) na kuwapeleka Dodoma kupokea kadi za CCM chini ya mwenyekiti wa CCM Mkapa. Wanafunzi walahidiwa wangepatiwa ajira kwa kufanya hivyo. Hii ilimjenga sana Matayo ambaye aliisha kuwa maarufu kwenye ofisi za chama Dodoma, kama mjumbe wa NEC na mkutano mkuu. Mwaka 2000 aligombea Ubunge Same Magharibi na kushinda na kuteuliwa kuwa waziri mdogo. Wakti huu aliisha tamka kwamba amesomea Afrika Kusini digrii ya falsafa (PhD). Prof Msolla wakati aliyekuwa waziri wa elimu ya juu na sayansi ambaye aliwahi kufundisha SUA alimjua sana Matayo na alimwita Matayo na kumuuliza kuwa PhD alifanya lini na wapi na pia aletee PhD thesis yake. Prof Msolla alisema "Matayo aliogopa sana na alikili mbele yangu, kuwa Prof mimi nimetumia hii title kisiasa zaidi, sina MSc wala PhD”1.





 
  
Kashfa ya vyeti bandia

Dr Mathayo ni mmoja wa wabunge vijana waliochaguliwa na Raisi Kikwete kuwakilisha ngwe yake ya "Nguvu mpya" kama naibu waziri. Katika awamu hii Kikwete alionekana amechagua vijana wenye vipaji na elimu. Vyeti vya Mathayo's zimeleta kizaazaa tangu alipochaguliwa kwenye uwaziri mwaka 2005. Matayo alihitimu chuo kikuu cha Kilimo (SUA) mwaka 1997 kama daktari wa mifugo. Baada ya hapo alitoka nje ya nchi kwenda kutafuta ajira Botswana ambako aliajiriwa na serikali ya Botswana kama mwalimu kweny chuo cha kilimo huko Serowe. Mathayo anadai kwa mwaka huo huo alianza digrii ya MSc 1998-2001, halafu PgDip (2000-2001), na PhD (2001-2003). Watu wengi wanaomfahamu ikiwa ni pamoja na waalimu wake wa SUA wanashangaa Mathayo aliwezaje kusomea vyeti vyote hivyo kwa muda wa miaka mitano huku akifanya kazi kama mtumishi wa serikali Botswana? Pia kashfa kwamba alikuwa akipokea mishahara miwili ya uwaziri na utumishi wa serikali ya Botswana haijajibiwa hadi leo.