Jumatatu, 24 Machi 2014

RAIS KIKWETE ASEMA SERIKALI TATU INA MAPUNGUFU






RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelihutubia Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma na kulizinduwa rasmi, huku akionekana wazi wazi kupinga mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu yake iliyowasilishwa kwa wabunge.

Akizungumza kwa hisia Rais Kikwete ameukosoa mfumo wa Serikali tatu kwa madai kuwa Serikali hiyo ya Tatu ambayo ni ya Muungano wa Tanzania itashindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha kwa kuwa itakuwa haina vyanzo vya mapato vya uhakika na kutoseleza utekelezaji uendeshaji.

Alisema Serikali washirika yaani Tanganyika na Zanzibar ndizo zitakazokuwa na vyanzo vya mapato na rasilimali hivyo endapo upande mmoja wa washirika utagoma kuchangia fedha kwenye Serikali ya Muungano Serikali hiyo itakosa uwezo “…Lakini mtambue uamuzi usiokuwa sahihi kwa jambo hili (Serikali 3) unahasara kubwa,  kuingiza nchi yetu kwenye matatizo na kuwa na mazingira magumu, vurumai na yote tuliojenga kwa nusu karne yakapotea” alisema Rais Kikwete.



Aidha hoja  zilizopo katika rasimu ambazo ameonesha wasiwasi ni uwepo ukomo wa kugombea ubunge, wananchi kuwa na mamlaka ya kumvua mbunge wao kabla ya kipindi cha uchaguzi na rasimu kukataza wabunge kuwa mawaziri. Akifafanua zaidi alisema wapo watu wanaweza kutumia vibaya uamuzi huo hivyo kuanzisha vitina na kujikuta wananchi wanampinga mbunge wao ili aondoke na kuhusu ukomo wa ubunge utawanyima watu fursa za kuwatumikia wananchi.

Alisema hata takwimu zilizotolewa na tume kwamba Wananchi wanaotaka Serikali tatu ni wengi na Serikali tatu haiepukiki zina ulakini hivyo kuwataka wajumbe wa bunge hilo kuhakikisha wanaleta katiba itakayo kubaliwa na wengi na si kukataliwa na wananchi kwenye kura za maoni hapo baadaye.                                                                 




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni