2 Aprili, 2014 - Saa 09:31 GMT
Watu wawili wamekamatwa baada ya kupatikana wakiwa na maguruneti mawili nyumbani mwao wakati polisi wakiendelea na msako mkali mtaani Easteligh nchini Kenya.
Polisi wamekuwa wakifanya msako katika mtaa huo wa Easteligh tangu mashambulizi ya maguruneti kuwaua watu 6 Jumatatu usiku na kuwajeruhi wengine 30.
Mkuu wa polisi alisema kuwa wawili hao walikamatwa pamoja na watu wengine 400 katika eneo hilo huku msako wa polisi ukiendelea.
Polisi wanasema kuwa wanawahoji wawili hao kuona ikiwa wanaweza kupata taarifa zaid.
Takriban watu 657 walikamatwa na polisi Jumatatu usiku mtaani Eastleigh, baada ya shambulizi la kigaidi dhidi ya mkahawa na kuwaua watu sita.
chanzo kutoka BBC SWAHILI 2 Aprili, 2014
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni