MSANII WA NYIMBO ZA INJILI WA WA WIKI
Karibu mpenzi msomaji na mfuatiliaji katika ukurasa huu wa mahojiano ya wasanii wa injili wanaotamani kuinuka katika tasinia hii ya muziki wa injili lakini kwasababu moja au nyingine au kutokana na changamoto mbalimbali hushindwa kutimiza malengo yao, katika ukurasa huu tunafanya mahojiano wasanii wachanga wanaotamani kuinuka na walioonyesha nia ya kweli ya kutamani kujikita katika injili kwa njia ya uimbaji, karibu sana na fuatana na mimi mwanzo hadi mwisho.
Katka ukura6sa huu leo nina mleta kwenu msanii wa nyimbo za
injili kutoka katika kanisa la MARANATHA RECONCILIATION CHURCH – MANZESE kwa
jina anatambulika kama PRISCA FRANK
MAGOMA anasifu na kuabudisha kan kanisani ambapo timu ya mwangaza media
ilimshuhudia akiiendesha huduma hiyo kanisani kwao na kuamua kumfuatilia kujua mengi kuhusu
tasinia hii timu ya mwangaza media
iliamua kumtembelea kazini kwake
na kufanya mahojiano nae kuhusu mambo mengi sana katika tasinia hii ya injili
(kwa njia ya uimbaji) ambapo hadi hivi sasa albamu
yake ya nyimbo nane ipo studio kwa ECK
PRODUCTION magomeni mwembechai
PICHA ZOTE NI PRISCA .MAGOMA AKIWA KAZINI KWAKE MAGOMENI POPOBAWA BARABARA YA SINZA KUPITIA TANDALE UZURI NDANI YA ROBIN PHOTO STUDIO& GRAPHICS DESIGN
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Kwa jina naitwa PRISCA FRANK MAGOMA , Nimezaliwa Tarehe
09-12-1983 ni mtoto wa pili kati ya
watoto sita wa mzee Magoma ni mzaliwa wa mkoa wa KILIMANJARO wilaya ya SAME.
Elimu yangu ni kidato cha nne katika shule ya sekondari ya
MSAKI MEMORIAL ya kibamba jijini Dar es salaam.
Nimeolewa na nina watoto
wawili tangu mwaka 2006 ambapo kwa muda
wote huo nipo katika ndoa kipindi tunaoana na mume wangu alikuwa anafanya kazi
ya ualimu katika wilaya ya KIBAHA VIJIJINI
kisha baadae tulihamia DAR baada ya mume wangu kuamua kuacha kazi na
kuamua kuingia kwenye ujasiriamali.
Ambapo kwa sasa tupo Dar na kazi
yetu ni biashara kama mnavyoniona hivyo hapa nipo ofisini kwangu. “alisema dada
Prisca”
MALENGO YAKE
Kwa ujumla malengo yangu ni mengi ila ufupi
=== Niweze kufanya
kazi ya mungu kwa utimilifu kupitia nyimbo za injili.
=== kuwa na familia inayompenda mungu na kutenda mapenzi ya
mungu
KUHUSU ALBAMU YAKE
Albamu ipo studio kwa ECK PRODUCTION magomeni mwembechai
inaendelea kutengenezwa siwezi kusema imefikia hatua gani ila ipo karibu sana kutoka nategemea kazi itakuwa nzuri sana wapernzi wa mziki wa injili wategemee kitu
kizuri na mabadiliko makubwa katika
tasinia hii ya muziki wa injili.
CHANGAMOTO KATKA TASINIA YA NYIMBO ZA INJILI
Changamoto ni nyingi ila zilizochukua uzito ni gharama za maandalizi ya albamu studio
kiasi kinachotakiwa ni kikubwa kiasi
kwamba waimbaji wengi hasa wanoibukia
wan ashindwa kumudu, pia kwa wengine ipo changamoto ya rushwa ya mapenzi kwa waandaaji wa mziki wa injili na
wasambazaji wa mziki huu. Zaidi ya zote kwangu mimi ni wizi wa kazi za wasanii unaoendelea katika maeneo mengi ya jiji na hata mikoani ni vyema wanaofanya wizi huo waache kwani ni dhambi kufanya hivyo na inamnyima mapato msanii na serikali pia inakosa kodi.
Ahsannte ndugu mpenzi wa kurasa hii ya m,sanii wa wiki kupitia MWANGAZA MEDIA tangu mwanzo wa mahojiano nakusihi endelea kufuatilia ukurasa huu utapata mengi sana na kwa wale wanaopenda timu ya MWANGAZA MEDIA iwatembelee waendelee kutembelea ukurasa huu hapo baadae tutatoa fomu maalumu ya maombi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni