Takwimu kupitia wizara husika inayohusiana na maswala ya utalii inaonyesha idadi ndogo sana ya watanzania wanaotembelea mbuga za wanyama na hata sehemu zingine za utalii hapa nchini tofauti na wageni watokao Nchi za mbali hasa Ulaya (Uingereza,Ujeruman Ubeligiji) Marekani, China na nchi nyingine kote Duniani.
Utafiti uliofanyika unaonyesha sababu zifuatazo ni chanzo cha wananchi wa Tanzania katika sehemu kubwa
kutothamini utalii
1.Hawajui utalii ni kitu gani?
2.Hawajui ni umuhimu wa utalii
3.Wanashindwa kumudu gharama kwani gharama za chakula na malazi ni kubwa
4.Ugumu wa maisha
5.Umbali hadi kufika sehemu za utalii.
6.Kutothaminiwa kwa watalii wandani na watoa huduma.
Shime Tanzania nchi nzuri yafaa sasa kubadilika na kwenda na mfumo mpya wa maisha kwa kupenda na kuthamini utalii wa ndani kuleta michngo ya nini kifanyike kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii ili Tanzania yetu isiwatoe tu ushamba wazungu bali na sisi Wazawa.
Elimu ya utalii inayotolewa mashuleni kuanzia ngazi ya chini IBORESHWE ili iwe ya kumjenga mtanzania atambue umuhimu wa utalii katika maisha yake ya kila siku katika ngazi zote za elimu Tanzania.
Pia imefika muda sasa Tanzania kutumia utalii kutangaza utaifa kama njia mojawapo ya kutuunganisha na kuwa kitu kimoja kama ilvyokuwa hapo zamani kwa kuwa na vazi la Taifa

![]() |

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni