Hotuba ya Jaji Warioba yapongezwa na Wajumbe CCM

Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge la katiba kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameipongeza
hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Hayo yamejitokeza pale mjumbe Seleman Jafo, alisema Jaji Warioba ameibua vitu
vingine ambavyo hajawai kuvisikia tangu awe mwanasiasa na kwamba msimamo wake
mpaka sasa ni kusimamia ukweli bila kuangalia maslahi ya Chama chake
anachotoka. Alisema pia Jaji Warioba ameweka wazi na kufanya mustakabali wa
taifa hili unaweza kwenda sehemu ambayo sio nzuri endapo hatua za haraka
hazitachukuliwa kuhusiana na suala hilo
la Muungano.
Paulo Kimiti alisema kuwa licha ya kuunga mkono hotuba ya Jaji Warioba, lakini
vitu alivyoeleza vyote ni vya msingi katika mustakabali wa Taifa.Alisema kwa
mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010,
kutambua Zanzibar
ni nchi huru ndani ya Muungano kunaufanya Muungano kuwa wa nchi mbili na
serikali mbili badala ya nchi moja.
Kimiti alisema kinachopaswa kufanywa sasa na wajumbe wa bunge hilo ni kujadili rasimu bila ushabiki wa
vyama na makundi.
Innocent Kalogeris, Mbunge Morogoro kusini, CCM alisema taarifa aliyotoa Jaji
Warioba inadhihirisha udhaifu wa uongozi kwani tayari katiba imevunjwa, lakini
kinachotakiwa ni kufanya marekebisho ya kusaidia kuimarisha Muungano na sio
kuanzisha Serikali tatu.
Ezekiel Maige, alisema Rasimu iliyowasilishwa inahitaji kufanyiwa marekebisho
makubwa na Bunge hilo kwa kuwa haijaziba mianya
ya upotevu wa rasilimali za nchi.Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania,
zimeunga mkono hotuba ya Jaji Warioba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni